• Sat. Apr 20th, 2024

UASU Yatishia Mgomo Baada ya Makubaliano yao Kukiukwa

Aug 20, 2021
324 300

Chama Cha wafanyikazi wa vyuo vikuu UASU kimetoa makataa ya Siku Saba kwa vyuo vikuu kutekeleza Makubaliano ya Mwaka 2017/2021.

Chama hicho kimetishia kuenda kwenye mgomo iwapo mishahara yao yote na mkataba waliotia sahihi miaka mitano iliyopita haitalipwa.

Mkataba huo waliotia sahihi mwaka 2017 unakamilika kabla ya matakwa yao kushughulikiwa.
Kulingana na mwenyekiti wa Kitaifa wa UASU, Bi Grace Nyongesa, Viongozi wa Vyuo vikuu wamefeli kutekeleza kile wanachopaswa kufanya.

“Tuko hapa kwa sababu Mkataba wetu wa 2017/2021 haujatekelezwa ipaswavyo na Wafanyikazi wa Vyuo vikuu wameendelea kufanya kazi. Tunahuzunika Sana na jinsi ambavyo Uongozi wa Vyuo unapuuzilia matakwa yetu. Tukijaribu kusema lolote, tunatishiwa”alisema Bi Nyongesa.

Viongozi wa chama cha UASU Wakitoa ilani ya siku 7 kwa Serikali Katika Hoteli Moja Nairobi PICHA/Jacktone Lawi

Akizungumzia mapema hii leo, katibu Mkuu wa UASU, Bwana Constatine Wasonga amesema Kuwa vyuo vikuu vinaenda kinyume na maagizo ya mahakama ya Ajira hapo Januari 15 ambalo liliagiza kutekelezwa kwa mkataba huo.

Aidha Bwana Wesonga amewataka ‘Machansela’ hao kujiuzulu iwapo pesa hazipo kwa Kuwa UASU haina uwezo wa kuwafadhili na pesa.

“Tumekubaliana sote kwa kauli moja Kuwa baada ya Siku Saba iwapo matakwa yetu hayatakuwa yamesgughulikiwa basi tutaenda kwenye mgomo wa Kitaifa. Hapatakuwepo masomo baada ya Siku Saba hizo. Pesa hizo Billioni nane nukta nane zilifaa kupeanwa zote Mara moja Wala sio kwa vipindi au mgao wowote. Hii no kinyume Sana na maagizo yaliyotolewa na Korti Januari,” alisema Wasonga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *