• Sat. Apr 20th, 2024

Tanzania Kuzindua Safari Za Ndege Kenya Mwishoni Mwa Mwezi

Nov 19, 2021
508 300

Ubalozi wa Tanzania Kenya umetangaza Kuanzishwa kwa safari za ndege kutoka Dar-es-Salaam hadi Nairobi. Uzinduzi rasmi unatarajiwa tarehe 26 mwezi huu. Ndege ya Kwanza itatoka uwanja wa Julius Nyerere International Airport Saa Kumi na Moja Unusu na Kuja Uwanja wa Jomo Kenyatta saa kumi na mbili na dakika arubaini na tano ambako safari zitazinduliwa rasmi kabla ya ndege hiyo kurudi Tanzania saa moja na dakika arubaini na tano.


Haya yanajiri baada ya biashara baina ya nchi hizi mbili kuimarika. Akitoa habari hizi kwenye ubalozi wa Tanzania Kenya, Balozi John Stephen Simbachawene amesema kuwa Kampuni ya ndege ya Tanzania Air Limited ndege aina ya Air Bus A220-300 ndizo zitakazo tumika katika safari hizi.


Tarehe tano na Nne Mei wakati wa ziara ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mara ya kwanza nchini Kenya walizungumza na Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta na Katika mazungumzo yao waliahidi kuimarisha mazingira ya biashara na Mahusiano baina ya Kenya na Tanzania. Uzinduzi huu ni matokeo ya Ziara na Mazungumzo baina ya Marais wetu. Kuboreka kwa biashara baina ya nchi zetu ndiko kumesababisha Uzinduzi wa safari hizi.


“Gharama za usafiri wa safari moja itakuwa Dola 210 za kimarekanina Safari za kuenda na kurudi itakuwa ina gharimu Dola 334 za Kimarekani kwa wastani elfu thelathini shilingi za Kenya. Patakuwa na huduma kama vile viburudisho, vitafunio kama vile Maji, Chai, Korosho na baadhi ya Korosho ni zile za Tanzania,” alisema Balozi.


Aidha balozi aliongeza kuwa abiria watakuwa na nafasi ya kulipa tiketi moja na kuenda miji mingine ya Tanzania. Pia, wale watakaotaka kuenda nchini jirani za Tanzania watafanya vile.


“Wasafiri watakuwa na fursa ya kupanda ndege za ndani kama vile Kuenda Zanzibari. Miji tisa itaunganishwa katika safari hizi. ikiwemo, Mwanza, Dodoma, na zinginezo. Tumetoa nafuu ya kuweza kukata tiketi moja na kuunganisha miji hiyo. Kutakuwa pia na safari ya kuenda nchi zinazo zunguka Tanzania. Abiria watakubaliwa kubeba mizigo ya uzani wa kilo 46. Tutakuwa tumewapa wafanyibiashara nafasi ya kufanya shughuli zao vyema,” aliongeza.


Alisema Kuwa ndege kubwa zitatumika kwa Kuwa idadi ya watakao Kuwa wakisafiri ni wengi mno baada ya kuimarika kwa biashara. Inatarajiwa safari mbili kwa Siku. Aliongeza kuwa ndege ndogo ndizo zinazotumiwa katika kuwasafirisha watu katika Miji midogo.

READ ALSO:Diamond Ventures Into Tanzanias’ PSV Business

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *