• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Shughuli zarejea Makao Makuu ya KNUT baada ya mnada

Jul 6, 2021
596 300

Oparesheni katika Chama cha waalimu KNUT zimereja siku chache tu baada ya wale auctioneers kufika katika makau makuu na kuchuku baadhia ya mali zao.

Kulingana na katibu mkuu wa chama hicho Collins Oyuu swala hilo lilienezwa bila kuzingatia maswala mengi na si kwamba oparesheni zao zililemazwa kabisa kwani hata baada ya mali hizo kuchukuliwa walikuwa wanatoa haduma za lazima kwa waaalimu.

‘’Nataka kuweka wazi kuwa tumekuwa tukitoa huduma na kwamab wale ambao walikuw wansema muungano huu umepigwa mnada ni uvumi mtupu na waalimu wamaknike.’’ Alisema.

Amesema kuwa ofisi yake imeanza mikakati maalumu kuhakikisha kuwa zile tarakilishi na baadhi ya viti vilivyochukuliwa vinarejeshwa lakini kufikia sasa wamerejesha hudumu zote.

Aidhaa amekubali kuwa chama hicho kimekuwa kikishudia uhaba wa fedha kuendeleza majukumu yake lakini tayari wanashirikisha tume ya kuajiri waalimu TSC kuhahakikisha kuwa wale waalimu waliondolewa katika rejesta ya knut wamerejeshwa.

‘‘Kwa sasa tumeanza mazungumzo na TSC na hivi karibuni mtaona mabadiliko katika chama hiki ..kitakuwa historia ya kiepkee,lazima wanachama wetu wa warejeshwa wote na hata pato la kila mwezi la chama,’’ aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *