Mwenyekiti wa muungano wa wanabodaboda Nchini [BAK] Kevin Mubadi amesema kuwa visa vya wanachama wake kusumbuliwa katikati ya jiji la Nairobi vimerudi tena.
Akizungumza na Taarifa News, Mubadi amesema kuwa hawana uhakika iwapo ni askari wa kaunti ya Nairobi ambao wameanza kuwasumbua kwa kuwa majuma kadhaa yaliyopita walimnasa Askari wa jela wakiwashika Vijana wa bodaboda na kuwaitisha hongo.
“Wanachama wetu wameanza kulalamika kusumbuliwa na askari wa baraza la jiji na hatuna uhakika kama ni wao kwa kuwa majuma kadhaa yaliyopita tuliwashika askari wa jeshi na Jela hapa katikati ya Jiji wakiwahangaisha vijana wetu,” alisema Mubadi.
Aidha ameomba iwapo kuna kiongozi ambaye ameanza kuwachochea askari wa baraza la jiji kuanza kuwahangaisha wanabodaboda kukoma kwa kuwa Jijini Nairobi huwa hapana mwelekeo wa ni wapi wanabodaboda wanfaa kuegeza bodaboda zao wanapofanya kazi.
Amesema kuwa, wao wenyewe ndio hushughulika na kujitafutia pahali pa kufanyia kazi lakini huwa wanahangaishwa sana.
Ameitaka serikali ya Kaunti kutimiza ahadi yao ya kuwaonyesha pahali pa kuegesha bodaboda zao ili kukoma kuwasumbua.
Ameongeza kuwa mtu huyu ambaye anadaiwa kuleta mahangaiko haya kuwakomesha askari wake kuwasumbuwa wanabodaboda, kwa kuwa walikuwa na mazungumzo kati yao na Jenerali Mbadi ya kuwalinda wanabodaboda wanaohudumu katikati mwa jiji.