Watetezi wa Wafanyikazi wa Ngono Wametoa Ripoti ya kwanza kabisa ya madhila, Vitisho, Mashambulio na vurugu ambazo Wafanyikazi wa Ngono hupitia.
Ripoti hii iliyohusisha Wafanyikazi 350 katika nchi 20 na inahusisha kesi za kukamatwa, unyanyasaji wa kijinsia kizuizini, uvamizi wa nyumba na Ofisi zao shinikizo lq kisolojia, Vitisho kutoka kwa Mameneja kazini pao, Familia, Wateja, Mashambulizi ya mwili, ufuatiliaji na askari katika kazi zao,kampeni na Kashfa za umma, mzigo wa kifedha, Ubaguzi, na Mambo mengine mengi.
” Katika mahojiano tuliyoyafanya katika vyumba vya kuishi, vitu vya magari ya Moshi,misikiti,makahaba,Sehemu za ususi,hoteli Maghala, boti, fukwe, na zahanati watetezi wa Wafanyikazi wa Ngono walipata ya Kuwa Wafanyikazi wa Ngono hudhulumiwa kutumia sheria na ubaguzi kupitia Sera za nchi tofauti,” alisema Erin Kilbride.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mwenyekiti wa Wafanyikazi wa Ngono katika Bara La Kenya Carolyn Njoroge amesema Kuwa Mara mingi wanahabari hutoa habari zisizo za kimsingi kuwahusu jambo ambalo huwakasirisha mno.
Aidha Ogutu ambaye ndiye msimamizi wao Bara La Afrika amesema kuwa wao wangependa kazi hii Yao iwache kufanywa haramu kwa Kuwa wanatumia viungo vyao tu Kama vile watu wengine wa kawaida.
“Tunatumia viungo vyetu tu Kama wale ambao hukimbia, huimba na wote wale hutumia viungo vyao kupata pesa. Tumeajiriwa tu Kama watu wa kawaida,” alisema Njoroge.