• Mon. Dec 5th, 2022

Rais Angazia Ufisadi Katika Wizara ya Afya-Gitali

Mar 29, 2022
157 300

Mwenyekiti wa Shirika la Kudhibiti matumizi ya Tobacco(KETCA) Joel Gitali amekashifu ufisadi katika wizara ya afya na wizi unaondelea kuripotiwa katika Shirika la KEMSA mwaka mmoja tangu Kashfa ya kwanza iliporipotiwa.

Kulingana na Gitali, bubadhirifu unaoendelea katika shirika hilo umewafanya washirika na wasaidizi wa ughaibuni kujiondoa.

“Ni jambo la kusikitisha jinsi wizara ya afya na taasisisi za Kiafya zinavyo shuhudia uporaji. Ni jambo la kusikitisha kuwa KEMSA limekuwa ni shirika ambalo limeporwa mno na watu wanaojitajirisha mno pasipo kujali maslahi ya wakenya. Shirika hili limewekwa pale kuhakikisha wakenya wanapata dawa zinazofaa kwa bei nzuri lakini wengine wamechukuia kama mradi wa kupata pesa za haraka,” alisema Gitali.

Gitali alisema anashangaa ni kwa nini ripoti haijawahi kutolewa na Rais alivyoahidi mwaka uliopita mwaka mmoja baadaye.

“Badala ya ripoti kutolewa, tunazidi kupata habari zaidi ya jinsi ambavyo shirika hilo linavyo endelea kushuhudia ubadhirifu,” aliongweza.

Aliita Serikali kuwatia Mbaroni na kuwashtaki washukiwa wakuu kwa kuwa wanajulikana ili kuzuia washirika wanojihusisha na KEMSA na wizara ya Afya kujiondoa.

Kiongozi huyu amesema kiuwa ruwaza ya mwaka 2030 haiwezi kuafikiwa iwapo sisi wenyewe ni maadui wa ajenda hii inayokumbwa na vikwazo vingi.

Aidha, Gitali amesema kuwa wagonjwa wa Saratani ambao baadhi ni waathiriwa wa matumizi ya ya Tumbaku kwa sasa wamo mashakani kwa kuwa vifaa vingi vinavyotuiwa katika matibabu yao haviwezi kurekebishwa wakati huu ambao washirika katika sekta ya afya wanajiondoa nchini Kenya.

“Washirika wetu wa kimataifa wanaondoka kwa kuwa ubadirifu mwingi unaendelea. Ni jambo ambalo tunalilia kwa kuwa kila siku huwa tunawalilia wagonjwa wa Saratani waweze kusaidiwa. Kwa sasa siasa zimenoga na watu wanajali tu maslahi yao. Hawa wanaopaswa kusaidia serikali yetu iendelee kupata misaada ndio wanaoendeleza wenaotupennda na kusimama nasi kujiondoa,” aliongeza Gitali.

Ameiomba serikali kupunguza makali ya kisiasa na kuangazia ufisadi unaondea katika wizara ya Afya kabla ya mengi kuendelea kutukia katika wizara hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *