• Fri. Apr 19th, 2024

Raila Ataka Wakenya Kuendeleza Uongozi Mzuri Ulioachwa na Kibaki

Apr 30, 2022
418 300

Mgombea urais kupitia tiketi ya muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga ameungana na waombolezaji nchini kumpa buriani hayati rais Mwai Kibaki katika sherehe ya mazishi iliyofanyika mjini Othaya kaunti ya Nyeri.

Raila amemuomboleza Kibaki kama kiongozi aliyechangia pakubwa wajumbe wa bunge la kitaifa kutupilia mbali kipengele cha 2A cha katiba ya awali na kuruhusu ujio wa vyama vingi nchini.

Odinga amesema uongozi bora uliojawa na maono na ari ya kuleta mabadiliko nchini ni baadhi ya yale yaliompelekea kuunga mkono azma ya marehemu Kibaki kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi wa 2002.

Huku akiwataka wakenya kuendeleza uongozi bora uliowachwa na Kibaki, Odinga amemtaja marehemu Kibaki kama kiongozi aliyehakikisha taifa linaimarika kupitia miundo msingi nchini ikiwemo ujenzi wa barabara kuu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *