• Fri. Apr 19th, 2024

Raila Ameniidhinisha Kuwania Ugavana Nairobi –Tim Wanyonyi Asema

Oct 22, 2021
238 300

Mbunge maarufu wa  eneo bunge la Westlands Tim Wanyonyi Sasa anasema kuwa Yuko tayari kabisa kinyanganyiro cha ugavana Nairobi.

Kulingana na Wanyonyi amewasiliana na kinara wa ODM Raila Odinga Kuhusu azma yake ambaye amempa idhini ya kutafuta kura.

‘‘Ni kweli kuwa nimepata idhini kwa Baba nilipoenda kwake aliniambia kwamba niende nionge na wananchi na tunapozungumza hakuna aliyejitangaza kuwa anataka kiti cha ugavana  katika chama cha ODM.’’ Wanyonyi aliwambia wanahabari.

Wanyonyi ameapa kufanya mabadiliko Cityhall akitua kiti hicho.

‘‘Nimekwepo Cityhall nina uwezo wa kuhakikisha kuwa zile mabilioni tunapata katika bajeti zimetumika kwa njia sawa,nia yangu kubwa ni kuimarisha miunda msingi,nafasi za kazi  na hata kuimarisha elimu ya watoto wetu.’’ Wanyonyi alidokeza.

Alikua anaongea Ruaraka na jammii ya Mulembe ambapo pia amewahimiza kuchukua kura.

‘‘Kwa jamii yangu lazima mnishike mkono kwanza na mniidhinishe nikitoka hapa naenda kwa makabila mengine nikiwa na nguvu nanyi mlinde boma …ndio maana ni muhimu tukiwa na kura zetu na tuzipige ..hapa Nairobi pekee tuko na  watu laki  nane.’’

Ikiwa atapata  tiketi ya chama cha ODM  Tim atapambana na Margret Wanjiru wa UDA debeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *