Polisi hapa Nairobi wametaka wananchi kufuata kanuni za Covid 19 haswa kafyuu kwani hawatalegeza kamba katika juhudi zao za kuhakikisha kanuni hizo zinafwatwa.
Wengi walijipata pabaya Jumamosi hii ni baada ya barabara kuu ya Thika kuwekewe vizuizi baada ya saa nne usiku.
Kulingana na kamanda wa polisi Kasarani Peter Mwanzo wataendelea kuweka roadbloaks hizo, kuhakikisha kuwa wale wanaokiuka sheria wanaandamwa.
‘‘Tulipata mwelekeo kuwa aina ya ugonjwa huu sasa ni hatari na ni lazima wakenya wafwate masharti na kanuni zote za ugonjwa huu na kwamba sisi tuendelea kuhakikisha kuwa tumewandama watakaokikua sheria hizo.’’ Mwanzo alisema.
Ameongeza kuwa imekuwa vigumu kudhibiti barabara hiyo ya Thika road kwa sababu ya uzembe na kutosikia kwa wakenya huku wengi wakikosa kuheshimu kanuni za Covid, haswa masaa ya kafyu.
‘‘Wakenya ni wasumbufu sana ukizingatia msongamanoi ulishuhudiwa ni watu ambao hawaskizi na hawaelewi chochote..lakini hatutakoma tutaendelea kuweka vizuizi na wanaotoa hudumu muhimu tutawelekeza.’’ Mwanzo aliongeza.
Msongamano ulishuhudiwa katika barabara ya Thika siku ya Jumamosi baada ya polisi kuweka vizuizi kadhaa katika barabara hiyo.
Ilimlazimu kamanda wa polisi Nairobi Augustine Nthumbi kufika katika eneo hilo kakagua hali baadae vizuizi hivyo vilitolewe.
Wiki jana inspekta mkuu wa polisi Hilary Mutyambai aliotoa amri kwa jeshi la polisi kuhakikisha kuwa kanuni zote za Covid zimefwatwa kikamilifu.