• Sun. Jun 23rd, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Polisi Walionaswa Wakipokea Hongo Waadhibiwa

Jul 26, 2021
370 300

Maafisa wa Polisi wa kitengo cha Trafiki walionaswa katika video wakipokea rushwa katika barabara ya Kangundo wameadhibiwa na Tume ya Huduma za Polisi (NPS).

Kulingana na video iliyopeperushwa majuzi na runinga moja ya humu nchini, maafisa hao walionekana wakijadiliana na wananchi wawili wakidai kupewa hongo.

Kwenye video maafisa hao wa Trafiki walionekana wakiisimamisha Matatu katika barabara ya Kangundo na abiria wawili wa kiume na wa kike wakapewa hongo kwa niaba ya askari hao kutoka kwa mhudumu wa matatu.

NPS imesema imewatambua maafisa hao baada ya kupewa video hiyo na hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi yao. “

Kulingana na video ambayo imekuwa ikienezwa kote inayoonyesha maafisa wa Trafiki wakipokea hongo wakishirikiana na Wananchi katika barabara ya Kangundo.

“Tumeanzisha uchunguzi wa haraka ili kuwaadhibu maafisa hao,” ilisoma taarifa ya NPS.

“Maafisa hao watachukuliwa hatua kali za kisheria. pia Tunashukuru Runinga ya Citizen kwa kutoa habari hizo na kwa hivyo tunawahimiza wananchi kuripoti visa vyovyote kama hivyo na kuwaanika maafisa wanaochukuwa hongo kwenye magari.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *