• Mon. Mar 27th, 2023

Nusu mkate ya CDF asema mbunge wa mvita

Jan 27, 2023
62 300

Mbunge wa mvita Machele Mohamed Soud ametoa kauli yake kuhusu mgogoro unaondelea baina ya wabunge na serikali kuu kuhusu ugavi wa hela za CDF ambazo zinazotegemewa pakubwa na wanafunzi kutoka jamii zisizojiweza

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa katika hoteli Moja ya kifahari wakati wa kongamano la wabunge Machele amesema kwamba fedha walizopokea baada ya kususia vikao vya kongamano hazitoshi kamwe kufadhili masomo ya wanafunzi Takriban alfu tano mia Saba kutoka kidato Cha kwanza hadi kidato Cha nne.

Aidha mbunge uyo ametilia shaka kupokea kwa mgao uliobaki kwani imesalia tu miezi mitano ili kukamilika kwa mwaka wa serikali ivyo basi uenda Hela izo zisiweze kupatikana uku masomo yakisambaratika kwa ukosefu wa karo.

Fedha izo ni asili mia thelathini na Tano ambayo ni nusu za alizotarajia ivyo basi zitakwenda kwa masomo ya shule za upili uku wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi zinginezo wakisalia nje bila ufadhili wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *