Aliyekuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Raila Odinga yuko salama baada ya ndege aliyokuwa ameabiri kuhusika kwenye ajali baada yake kushuka.
Abiria wawili waliokuwa kwenye ndege hiyo aina ya Helicopter walinusurika na majeraha kiasi na wamepelekwa hospitali ili kupokea matibabu.
Kulingana na Msemaji wa Raila Denis Onyango, ndege hiyo Bell 407 Yenye usajili 5Y-PSM ilikuwa imemfikisha Raila shule ya msingi Kudhok eneo Bunge la Gem kaunti ya Siaya.
Raila alikuwa anaenda kujumika na Rais Kenyatta katika uzinduzi wa miradi tofauti tofauti.
Rubani wa ndege hiyo huko salama.
Katika taarifa, amesema kuwa ndege hiyo ilikuwa imeanza kupaa na ilikuwa Mita tano juu kabla ya kukumbwa na hitilafu ambazo ziliifanya kutua gafla.