• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Mwili ulio ibwa kwenye kaburi wapatikana kichakani

Jun 14, 2021
1,043 300

Mwili wa mwanamke uliokuwa umeibiwa kutoka kwa Kaburi eneo la mabirikani Mazeras Kaunti ya Kilifi umepatikana kilomita chache kutoka ambapo ulikuwa umezikwa.

Juma lililopita, familia Moja katika eneo la mabirikani ililazimika kuzika mgomba baada ya watu wasiojulikana kufika na kuiba mwili wa mama yao uliokuwa umezikwa.

Sababu za kitendo hicho hazijajulikana mpaka leo.

Akizungumza nasi, mjane, mme wa Mama aliyefariki aliwaomba waliouchukuwa mwili na jeneza kuregesha.

“Tunaomba wale waliofanya hiki kitendo wauregeshe mwili wa Mama. Hatujui ni kwa nini walifanya hivi. Tumelazimika kuuzika mgomba kwa kuwa Kaburi haliwezi kaa bure,”alisema mjane.

Familia hiyo sasa watauzika tena mwili huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *