418 300
Mfanyibiashara katika soko la Kagumu kaunti ya Kirinyaga, aliuawa siku ya ijumaa, kwa kudungwa kwa kisu na mwanamke wa umri wa makamu baada ya mzozo wa deni la elfu mbili.
Mwanawe Martin Kariuki, alisema babake mark Karimi mwenye miaka 45 alikufa alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Kerugoya.
Wakaazi waliokuwa wamejawa na ghadhabu walichoma bidhaa za mwanamke huyo wakisema kuwa Karimi alikuwa ashamlipa deni hilo.
Mwanamke huyo alikamatwa siku ya jumamosi na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kagumo Wakaazi wanasema hayo ni mauaji ya tatu kutukia katika juma moja katika eneo hilo.