Mwanamke mmoja katika eneo la kisume ameaaga huku wanawe wawili wakikimbizwa hospitalini baada ya kuangukiwa na Kuta za Shule ya Upili ya wavulana ya Kisumu.
Ukuta wa Shule hiyo iliyo kwenye barabara ya Kakamega-Kisumu ziliporomoka mwendo wa saa moja asubuhi hii leo na iliwaangukia watatu hao walipokuwa wakipita.
Turuphena Chitwa alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga ambako alifariki kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.
Mtoto mmoja ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya msingi ya Arya aliumia mkono wa ke wa kulia na mguu wa kushoto. Yule mwenzake alipata na majeraha kidogo.
Akizungumza na Taarifa News,Boniface Odero ambaye alishuhudia ajali hiyo amesema Kuwa walimwokoa mama huyo na wanawe lakini aliaga alipofikishwa hospitani.
“Ajali hii ilifanyika mida ya saa moja asubuhi hii leo na Mama huyo na wanawe wawili walikuwa wanapita. Tuliwaokoa kutoka sehemu hiyo na kuwakimbiza hospitalini lakini mama alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata,”alisema Boniface.
Kulingana na Wycliffe Otieno ambaye ni mkaazi wa eneo hilo, Kuta hizo zilikuwa zimeonyesha dalili za kuporomoka lakini wahusika walikuwa wamepuuza kuchukuwa hatua madhubuti.
” Lalama zangu ni kwa serikali ya kaunti ya Kisumu kwa sababu Kuta hizo zilikuwa zimeonyesha dalili za kuporomoka na hawakujali kuzirekebisha,” alisema Wycliffe.
Naibu wa Chifu katika eneo hilo la Kisumu Kaskazini amedhibitisha tukio hilo na kusema Kuwa watoto hao wapo katika hali nzuri kwa Sasa licha ya majeraha hayo.
Aidha ameongeza Kuwa wanajaribu kufanya uchunguzi ili kubaini aliyeaga Kama ni mama ya watoto hao.
Aidha Bwana Okello amewataka watu Kuwa makini wanapopita katika maeneo yenye Kuta ili kuzuia visa Kama vile wakati mwingine.