• Thu. Sep 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Mwanafunzi Apigilia Msumari kwa Kichwa cha Mwalimu

Jun 10, 2021
500 300

Maafisa wa Polisi katika Kaunti ya Kericho wameanzisha Uchunguzi ili kumkamata Mvulana wa Miaka 18 wa kidato cha tatu shule ya Upili ya Anaimoi aliyemjeruhi Mwalimu Mkuu kwa msumari kichwani.


Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekeleza unyama huo baada ya Mwalimu Mkuu kuamuru dawati lake kuchukuliwa mpaka atakapokamilisha deni la shilingi Elfu Saba za Karo.


Siku moja baadaye ndipo Mvulana huyo alikuja na kibao kilichokuwa na msumari wa na umgonga nacho kichwani.


Waliokuwepo wakati wa tukio hiyo walimkimbiza Mwalimu Mkuu hospitalini ambapo ametibiwa na kurudi nyumbani.

Inasemekana kuwa kijana huyo amekuwa akiwatishia Walimu kadhaa shuleni humo.


Aidha, kamanda wa Polisi katika Kaunti ya Kericho, Bwana Silas Gichunge amesema kuwa msako wa mshukiwa huyo unaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *