• Fri. Jan 27th, 2023

Mwanadada Anaya Pertson apoteza uwezo wa kuona baada ya kufanyiwa tattoo katika macho

Dec 7, 2022
2,736 300

Mwaka 2020 Anaya alifanyiwa tattoo katika jicho lake la kulia ili liwe na rangi ya blue kisha December mwaka huo huo akafanya tattoo nyingine jicho lake la kushoto liwe la rangi ya zambarau. Mambo yalienda vizuri lakini baada ya muda mambo yakaenda arijojo akaanza kuvimba usoni na maumivu kisha kuanza kupoteza uwezo wa kuona na kuna tishio akawa kipofu kabisa kwa mujibu wa madaktari na kuweza kupata athari nyingine

Anaya anayetokea Ireland ya Kaskazini, ameupasua pia ulimi wake kama sehemu ya kutaka kuzidi kuwa mrembo na kuvutia pia kujichora tattoo hadi usoni na kukitoboa baadhibya sehemu za mwili

Anaya ambaye ni mama wa watoto 5 , amesema mwanae wa miaka 7 awali alimuonya kuhusu tattoo za macho kuwa sio kitu kizuri na sasa anajuta bora angesikiliza ushauri huo

Kabla, ya kibao kumgeukia,Anaya alipata inspiration ya kufanya tattoo za macho toka kwa mwanamitindo Amber Luke toka Australia anayejulika zaidi kama “blue-eyed dragon” ambaye 2019 alifanyiwa tattoo za kuyafanya machonyake yawe ya blue kisha kupoteza uwezo wa kuona kwa wiki mbili

Swipe kumuona Anaya alivyokuwa kabla ya hizo tattoo za macho, na pia kumuona huyo role model wake(Amber Luke) kabla na baada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *