537 300
Walimu na wanafunzi katika shule ya Msingi ya Yanyonge Mwingi Kaunti ya Kitui waliachwa na mshtuko baada ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kujitoa uhai kwa kujinyonga.
kulingana na Walimu na wanafunzi wa shula hiyo, Mwalimu Mkuu kioko Mutie mwenye umri wa Miaka 46, alikuwa mchangamfu na hakuonyesha dalili zozote za kuwa na msongo wa mawazo.
Wazazi, Walimu na wanafunzi wamemtaja Mwalimu huyo kama aliyependa masomo Sana.
Aidha kilichomshinikiza kujitoa uhai hakijajulikana kwa kuwa hakuwacha ujumbe wowote wa sababu za kufanya vile.
Mwili uliondolewa na kupelekwa katika Makafani ya hospitali ya Kaunti Mwingi.