Mwakilishi wodi wa Kiagu kaunti ya Meru aaga dunia akipokea matibabu kule India.
Eunice Karegi alikuwa akipokea matibabu huko India ambako amekuwa akitibiwa Saratani.
Habari za kifo chake zilitangazwa mchana hii leo. Alikuwa Mwanamke wa pekee katika kaunti ya Meru kuchaguliwa kam mwakilishi wodi. Hili lilimfanya kuwa miongoni mwa viongozi ambao wanapigania usawa wa jinsia katika uongozi.
Alikuwa amechaguliwa kupitia chama cha Maendeleo Chap Chap chake Gavana Alfred Mutua.
Akimuomboleza Gavana Mutua amemtaja Eunice kama kiongozi aliyejitolea kuwahudumia wananchi wa kiagu kwa uaminifu.
“Natoa rambirambi zangu kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Eunice na chama chetu cha MCC. Amekuwa mwanachama mwaminifu, mwadilifu na mkamilifu,” alisema Mutua kwenye Twitter.
Mwili wa mwendazake unatarajiwa kusafirishwa nchini kwa ajili ya mipango ya mazishi. Mola ailaze roho yake mahala pema.