600 300
Mtu mmoja ameripotiwa kufariki hii ni baada ya makabiliano kuzuka Kati ya polisi na wakaazi wa Kahawa West.
Maandamano hayo yalisababishwa na ubomozi wa vibanda vya wakaazi hao.
Wakaazi wanasema kuwa vibanda hivyo vilibomolewa mwendo saa nane usiku wa kuamkia leo.
“Walikuja wakafanya ubomozi tukiwa tumelala saa hizi Kuna mtu hata amekufa kwenye maandamano..kile tunataka Sasa ni haki.” Mkaazi aliambia Taarifa News.
Aidhaa wameshtumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwani mali zao pia zimeibwa usiku baada ya ubomozi.
“Tumepoteza Mali ya maelfu baada ya wao kubomoa na kuenda …hasara tupu hapa.” Waliongeza.