Katibu mkuu wa chama Cha ODM Edwin Sifuna anasema kuwa chama Cha ODM kiko mbioni kuwasajili wanachama wapya hii ni baada ya kumpokea msaani Julius Owino Majimaji kama mwanachama wa ODM.
Kulingana na Sifuna tayari wameanzisha mipango maalum ya kuwasajili wanachama wapya bila malipo.
‘‘Kuingia kwa bwana Majimaji ambaye ni mtu amabye anajulikana ni vyema na sasa tumeanzisha mpango wa kuwasajili wanachama wapya kuhakikisha kuwa tumeimarika vilivyo kabla ya uchaguzi mkuu,’’ sifuna alisema.
Majimaji anasema nia yake kubwa ni kuhakikisha kuwa ameleta uongozi bora kwa chama na hata maendeleo .
‘‘Nimekuwa ODM lakini hii leo nimeingia ndani ya ODM rasmi kama mwanachama milele na kwamba ninachotaka kufanya ni kuhakikisha kuwa chama kimeimarika,uongozi bora lakni si siasa duni,’’ alisema.
Amesema kuwa lazima kila mmoja washikane mkono kuhakikisha Raila Odinga amepata urais.
‘‘Kama mwanachama wa ODM baba amejitahidi sana kupata kiti hiki hii ina maana kuwa tusichoke tuendelea kusimama naye tuhakikishe kuwa amekuwa rais,’’ alisema.
Hayo pia yametiliwa manani na naibu mwenyekitiwa chama hicho Ochieng Jera akisema kuwa Majimaji ndani ya ODM itainua hadhi ya vijana na hata sura ya chama.
‘‘Sijamjua leo ni mtu ambaye amekuza vijana wengi katika maswala ya burudani na kuingia kwake rasmi ODM ni ishara tosha kuwa tuendela vizuri kama chama na tumtaki kila la kheri akiingia katika kinyanganyiro cha ubunge Seme katika uchaguzi ujao.’’ Jera alisema.
Majimaji alilakiwa ndani ya chama cha ODM na Sifuna,Mbunge Tim Wanyonyi na viongozi wengine.