By Taarifa Team
Wakaazi wa Dandora 4 sasa wamepongeza unganishaji wa nguvu za umeme katika maeneo hayo.
Kulinganana na James Mbathi mmoja wa wakaazi hao wanasema kuwa mipaka ya mtaa huo wa Dandora 4 na Gomongo umeshuhudia visa vingi vya uhali kutokana na giza na kwamba umeme kwepo ni hatua kubwa kwa usalama.
‘‘Eneo hilo limekuwa hatari na kuwepo kwa stima itapunguza utovu wa usalam amabo tumekuwa tukishuhudia wengi wamedungwa kisu haswa wakati wakitoka kazini.’’ Mbathi Alisema.
Huku hayo yakijiri mwakilishi wadi eneo hilo Francis Otieno Ngesa ambaye amekuwa akiskumwa na mradi huo na kampuni ya Kenya Power ameshukuru kwa mradi huo, akisema ni hatua kubwa kwa maendeleo kwa wakaazi hao.
‘‘Nimekuwa nikifanya na Kenya Power kwa karibu ili tupate mradi huo na unganishaji huo utasadia pakubwa wakaazi..vijana wetu wamenyongwa sana katika eneo hili na pia tunataka maafisa wetu wa polisi kuhakikisha kuwa wao pia wamejitokeza na kulinda wananchi umeme peke hautoshi.’’ Ngesa alisema.