• Thu. May 19th, 2022

Mheshimu Amri Za Korti Wakili Wa Wafanyikazi Aambia Bunge La Nairobi

Nov 19, 2021

Wakili Bryan Khaemba wa  Wafanyikazi zaidi ya 30 wa Bunge la kaunti ya Nairobi walioshushwa vyeo na bodi ya Huduma za Bunge la Nairobi sasa ametaka uongozi wa Bunge la kaunti ya Nairobi kuheshimu amri za  mahakama na kukoma Kabisa kudhulumu Wafanyikazi kazi hao mpaka pale kesi iliowasilishwa itaskizwa na kuamuliwa.

Wakili Khaemba amesema Kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya Sheria na ni lazima bunge hilo liheshimu amri zilizotolewa.

Mahakama ya leba iliamuru bunge hilo kutowashusha vyeo Wafanyikazi hao mbali na kukata mishahara yao.

“Lazima sheria ifuatwe bunge hili pia liko chini ya sheria..wahusika wote wasipofanya hivyo basi tutarejea mahakamani wafungwe mwezi sita hatubembelezi mtu yeyote ni sheria.” Khaemba alisema.

Kumekuwa na malalamishi Kuwa Kuna baadhi ya Wafanyikazi kumi Kati Yao ambao walidaiwa kufutwa Kwa madai ya kufika  ofisi ya kaimu  karani wa bunge Adah Onyango japo bado bodi ya Huduma za Bunge haijadhibitisha.

“Wakati watu  wakilumbana katika eneo kama bunge basi ni Mwananchi ndiye anaumia tutajaribu njia zote kuhakikisha kuwa ikiwezekana pia tunaweza kuisuluhisha nje ya mahakama…lakini la muhimu kwanza ni Sheria kufuatwa kikamilifu na pande husika ikiwemo bunge hilo.” Khaemba aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published.