• Sat. Oct 12th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Mchakato wa Kurekebisha Katiba ni Haki ya Wanjiku si Rais wa Taifa –Wakili Shadrack Asema

Jul 2, 2021
274 300

Mawakaili wa maswala ya katiba wameendelea kujikuna kichwa kuhusu ikiwa rais Uhuru Kenyatta alikua huru kuanzisha mchakato wa BBI au la kwani ndilo swali linalowasumbua majaji katika mahakama ya rufaa.

Wakili Shadrack Wambui anahoji kuwa rais hangehusika kwa vyovyote kwani kama kiongozi wa nchi yuko na jukumu la kulinda katiba hiyo.

‘‘Rais kama kiongozi wa nchi ana jukumu la kulinda katiba na lakini si sawa yeye mwenyewe kuanzisha mchakato kwa sababu yeye ndiye mhifadhi wa katiba…kuanzisha harakati ya marekebisho ni jukumu la mwananchi wa kawaida mimi na wewe.’’ Wambui alisema.

Pia ameweka wazi kuwa kuhusika haimaanisha kuleta mswada wa  marekebisho ila  unahusika unapotoa pendekezo ama mawazo ya kurekebisha katiba lakini wakili Otiende Amollo alidokeza kuwa rais hakuhusika na ni mbunge Junet Mohammed na Denis Waweru ndiye aliyeongoza mchakato mzima kwani wao ndio walipeleka ripoti ya BBI kwa tume ya uchaguzi IEBC..

‘‘Kusema kuwa mchakato mzima unaanza unapounda mswada si kweli ,mchakato huanza unapopata  wazo na kutoa maoni kuhusu marekebisho na hivyo basi ni kweli ni rais ndiye aliyeanzisha mchakato huo ,ninachosisitiza zaidi ni kuwa kurekebisha katika na kura ya moni si vya kuchezea lazima mwananchi ahusishwe kikamilifu na sheria ifwatwe.’’ Aliongeza.

Kesi hiyo bado inaendelea katika mahakama ya rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *