• Thu. Sep 19th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

MCA wakashifu juhudi za kumuondoa Akuku Afisini

Jun 8, 2021
617 300

Wawakilishi wodi wa Kike wakiungwa mkono na wenzao wa kiume kutoka jamii ya Mulembe katika Kaunti ya Nairobi wamejiokeza vikali na kukashifu kitendo ambapo mwenzao Bi Sarah Akuku Pauline alivamiwa na Wawakililishi wodi wa Kiume katika ofisi yake hii Leo wakitaka kumng’atua mamlakani.

Akizungumza na Taarifa News Naibu Kiongozi wa Wachache katika Bunge Hilo,Bi Melab Atemah amesema kuwa wanakashifu kitendo hicho vikali kwa kuwa viongozi wale walifanya vile kwa tamaa zao za kibinafsi.

Aidha amesema kuwa wanaunga mkono Uteuzi wa Bi Pauline ambaye amekua akiwaongoza Nyakati ambazo mambo yamekuwa yakienda tenge na wakati wa misukosuko.


“Tunakashifu Wawakililishi wodi waliotekeleza kitendo hicho. Walifanya vile kwa tamaa zao wenyewe. Bi Akuku ni Kiongozi Mzuri kama tujuwavyo na amekuwa akitekeleza Kazi zake vizuri.”Alisema Bi Melab.

Aidha Mheshimiwa Ariviza amewataka wafanyikazi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi kutokuwa na wasiwasi kwa kupokea barua mbili. Amesema kuwa watafuata Sheria ipaswavyo na hawataki kuhangaishwa kwa kutolipwa kama mwaka uliopita kwa sababu ya viongozi ambao wanaleta vurugu katika Bunge Hilo.

“Tunajuwa sahi washaunda hela za kutosha na wanataka iwe kama mwaka jana ambapo watu walikosa mishahara yao kutokana na vurugu katika Bunge la kaunti hii. Wawache tufanye Kazi kwa amani,”alisema Bi Ariviza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *