• Thu. Apr 18th, 2024

MCA wa Mountain View Alaumu Mwenzake wa Kangemi Kuhusu Mipaka

Sep 25, 2021
837 300

Mwakilishi wadi wa Mountain View Maurice Ochieng’ sasa analaumu mwenzake wa Kangemi Paul Mhama kwa kuingilia kazi yake.

 Mahamba ameshtumiwa vikali  Kwa kutoheshimu eneo lake la  utawala na pia kutumia wafuasi wake kuvuruga mikutano ya kisiasa inayohusisha  Maurice eneo bunge la Westlands.

Hapo Jana wafuasi wa Mahamba walifumania Maurice katika mkutano na IEBC eneo la Kangemi na hata kujaribu kumzuia kuingia.

Mradi wa Barabara Mountain View PICHA/MAKTABA

 ‘‘Kitu kubwa amabyo inaleta shida kati yangu na Mahamba ni mipaka kwa sababu hajuui wadi yake inaishia wapi ..ni MCA wa Kangemi lakini unapata anafanya mamabo yake ya kisiasa kwa wadi yangu..juzi kulikuwa na waathiriwa wa moto tukaenda huko mpaka mbunge wetu Tim Wanyonyi kupeana vyakula yeye kumbe alishafika asubui hiyo na kuwaambia kuwa atwasadia ati mimi sisaidi Waluhya…siasa kama hizo hatutaki kabisa Mahamba anafaa kuhamasishwa kuhusu mipaka ya wadi yake.’’ Maurice alisema.

Mbunge Tim Wanyonyi Katika Wadi ya Mountain View

Maurice ametishia kumchukulia hatua ya kisheria ikiwa hata koma kuingia na kueneza siasa duni katika wadi yake ya Mountain View.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *