• Sat. Dec 9th, 2023

MCA wa Makongeni Asisitiza Matumizi ya Teknolojia Kwa Vikao Vya Bunge

Aug 5, 2021
229 300

Wawakilishi wadi wameendelea kutoa maoni tofauti kuhusu kuhudhuria mkutano na vikao vya bunge kupitia mfumo wa zoom.

Akizungumza na Taarifa News kiranja wa wachache Peter Imwatok anasema kuwa ni sawa wakihudhiria vikao kupitia njia ya kieletroniki kwani afya ni muhimu wakati huu wa ugonjwa wa corona.


“Sijui ni vipi Wakilishi wengine wadi wanamskuma Spika kufungua tena vikao kwa Wakilishi wadi ilhali idadi ya maambukizi inaendelea…maisha yetu ni ya muhimu wakati huu,” Imwatok alisema.


Aidhaa anasema kuwa matumizi ya teknolojia kufanya vikao yamefanya wengi wao kukumbatia teknolojia katika maswala mengi bungeni.

Kiranja wa Wachache katika bunge la county ya Nairobi Peter Imwatok


“Sisi kama Wakilishi wadi lazima tukumbatie teknolojia itasaidia pakubwa katika utendakazi wa bunge letu tumefanya mengi na wengi wanakumbatia.”aliongeza.


Kwa Sasa Wakilishi wadi wa Ngara Chege Mwaura, Francis Otieno Ngesa wa Dandora 4 wameshikilia kuwa vikao hivyo ni muhimu kufanywa moja kwa moja kwani wanapata fursa ya kuuliza maswali kwa urahisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *