• Sat. Oct 12th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

MCA Peter Imwatok Awachiliwa Huru Na Mahakama Katika Kesi ya Bunduki

Aug 24, 2021
322 300

Na Taarifa Team

Mwakilishi wadi wa Makongeni Peter Imwatok amewachiliwa huru  na mahakama ya Milimani  katika kesi ya iliokuwa ikimkabili kuhusu umiliki wa bunduki aina ya pistol bila kibali.

Jaji Carolyne Muthoni Njagi hajampta na hatiya kwani upande wa mashtaka ulifeli kutoa  ushahidi wa kutosha kuonyesha mshatakiwa alimliki bunduki hiyo kinyume na sheria.

‘‘Upande wa mashtaka haujawasilisha ushahidi kudhibitisha kuwa mshukiwa  alikua na cheti na hata leseni feki ya kumiliki silaha hiyo na hivyo basi korti hii imemwachilia huru.’’ Jaji NJagi alisema.

Imwatok alisahau bunduki hiyo katika mkahawa moja kule Industrial Area mwaka wa 2017 na baadae silaha hiyo  ilichukuliwa na polisi na akafunguliwa mashtaka.

Mwakilishi Wadi wa Makongeni Peter Imwatok Akiwa Mahakamani Leo PICHA/JACKTONE LAWI

Wakili wa Imwatok bwana Kokebe kwa upande wake ametaja uamuzi wa leo kama ya kihistoria kwani mteja wake, amekuwa akilipia leseni ya bunduki na kesi yenyewe ilikua na mskumo wa kisiasa.

‘‘Nimeipokea vyema uamuzi wa leo kwa sababu kesi hii haukuwa na uzito wowote jaji amedhibitisha kuwa mteja wangu haukuhusika kwa vyotevyote kwa mashtaka yote manne ikiwemo kumiliki bunduki bila leseni…..alikuwa na silaha kihalali na cha kushangaza amekuwa akilipia leseni yake kila mwaka.’’ Kokebe alieleza Taarifa News.

Upande wa mashtaka sasa una siku kumi nne kukataa rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *