Aliyekuwa Mbunge wa Kibwezi, Richard Kalembe Ndile aaga dunia na Umri wa Miaka 57.
Taarifa zinasema kuwa alikuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi kwa takribani majuma Matatu yaliyopita ambako amefariki akiwa.
Akitoa taarifa za kifo chake, mwanawe Anthony Kioko amesema kuwa Babake aliaga asubuhi mwendo was saa kumi na Moja na dakika thelatini na tano.
Kalembe ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Maji ya Tanathi amekuwa mgonjwa kwa muda sasa.
Alikuwa kimya tangu kushindwa kura mwaka wa 2017 katika eneo Bunge la Mavoko.
Kando na kuwa mwanasiasa, Kalembe amewahi kufanya Kazi katika kampuni za ujenzi na kuuza Changarawe na Mawe.
Katika mahojiano ya mwisho naye mwaka uliopita, alisema kuwa angewania ubunge wa Mavoko tena mwaka ujao.
“Niliwania ubunge kwa tikiti ya chama cha Jubilee mwaka 2017 na kupata kura 22000. Kama ningekuwa na makaratasi ningewania ugavana na kufanya Kazi zaidi ya magavana wengine,” alisema Kalembe.
Jamii nzima ya Ukambani wamempoteza Kiongozi aliyejitolea kuhakikisha mahitaji yao yanashughulikiwa ipaswavyo. Mola ailaze roho yake pema penye wema.