Mawakili wa maswala ya kisheria sasa wanataka vute ni kuvute kati ya tume ya uchaguzi nchini IEBC na bunge kusuluhishwa mahakamani.
Kulingana na wakili Shadrack Wambui ni mahakama pekee ambayo iko na kusuluhisho.
Kumekuwa na nipe nikupe kati ya bunge na tume ya IEBC kuhusu mwongozo mpya wa uchaguzi, bunge likishtumu IEBC kwa kutengwa.
Kulingana na Wambui ikiwa wabunge hawakuridhika na tendo la IEBC kuchapisha mwongozo za uchaguzi bila kuidhinishwa na bunge basi wangefika kortini lakini si kujigamba na kuamrisha tume hiyo kuondoa katika gazeti la serikali.
‘‘Bunge halina nguvu kuelekeza na kushurutisha tume ya IEBC kufanya jambo fulani na ikiwa hawajaridhika basi ni mahakama tu amabyo ina nguvu kuleta uwazi na mwongozo kuhusu sheria.’’ Aliambia Taarifa News.
Aidhaa ameshtumu IEBC kwa kudharua bunge na kuchapisha mwongozo hayo bila kuidhinishwa na wabunge.
‘‘IEBC pia lina nafasi ya kutunga baadhi ya mwongozo na hata sera lakini hayo pia lazima yaidhinishwe bungeni na ikiwa hawatafanya hivyo pia hilo ni ukiukaji wa sheria.’’ Aliongeza.
Mpaka sasa bunge limetishia kutopitisha mwongozo huo wa uchaguzi likisema kuwa halikuhusishwa.
Tayari mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati ameliomba bunge kufanya nao maridhiano ili mwongozo huo wa uchaguzi uidhinishwe lakini wabunge hawajakuwa na uwazi kuhusiana na ombi hilo la Chebukati.