Mawakili wa maswala ya kisheria sasa wametaka ,maafisa kutoka idara ya Mahakama kuheshimu sheria na kufika bungeni ili kujibu maswali kuhusu matumizi ya fedha.
Jaji mkuu Martha Koome hivi majuzi aliwaamrisha maafisa kutoka idara hiyo kutofika bungeni kujibu maswali hayo ya fedha akisema kuwa wanahanagishwa bungeni.
Lakini wakili Shadrack Wambui ametaka mahakama kuheshimu katiba kwani bunge lina mamlaka kisheria kufanya uchunguzi wao na hata kulinda mali ya wananchi.
‘‘Ni wajibu wao kuheshimu sheria hawawezijisimamia na bunge kumbuka kikatiba lina jukumu la kuhakikisha kuwa raslimali ya umma zimetumiwa vyema na ndio maana nasema lazima maafisa wa idara ya mahakama wafike bungeni na wajibike.’’ Wambui alisema.
Aliongeza ‘‘Pia ifahamike wabunge wamechaguliwa na wnaachji na kisheria wao ndio wanaopitisha bajeti ya seriali na idara zote ikiwemo mahakama ,wewe ukiwa unataka upewe bajeti na hutaki uulizwe matumizi yake basi wewe utakaa vipi?…Hakuna aliyejuu ya sheria lazima tukumbatie katiba yetu na tuheshimu sheria.’’
Kumemekuwa na nipe nikupe kati ya Mahakama na bunge huku spika Justin Muturi akimkashifu jaji mkuu Martha Koome kwa kutofuata sheria.
Spika Muturi ameweka wazi kuwa hivi karibuni atafiki idara ya mahakama ili waweze kutatau hilo.
‘‘Niliona kauli hiyo ya jaji mkuu kwenye mtandao wa kijami na nataka kusema kuwa idara za serikali hayafanyi kazi hivyo,nataka kusema kuwa tutawafikia na tutatue tatizo hilo kwa sababu kote dunia bunge linalinda mali ya serikali,na hata kutunga sheria kwa hivyo ni jukumu letu kuwaita kueleza matumizi yao.’’ Muturi alisema.