424 300
Mawakili sasa wamejitokeza na kupongeza uamuzi wa hapo jana wa majaji watano waliozima mchakato wa BBI ulionuia kubadilisha katiba.
Wakiongozwa na wakili wa haki za kibinadamu Shadrack Wambui uamuzi huo ni ushindi kwa wananchi walala hoi kwani shughuli ya BBI ilitekwa nyara na wanasiasa.
“Ni uamuzi wa busara kwani ilikosa mwelekeo siku ya kwanza pindi tu Rais aliunda jopo la kuisimamia…sheria inataka mwananchi kuianzisha haswa tukizingatia kipengele cha 257.” Alisema
Aidhaa anasema kuwa uamuzi huo pia itakuwa funzo kwa wale wanaonuia kufanyia marrkebisho katiba siku za usoni.