Mawakili sasa wameendela kutoa hisia mbali mbali kuhusu uamuzi wa jana wa BBI huku wengi wakipongeza mahakama ya rufaa kwa uamuzi huo wakisema kuwa katiba imelindwa.
Akizungumza na TaarifaNews wakili Shadrack Wambui anasema kuwa kulikuwa na njama fiche ya kuteka nyara idara ya mahakama kupitia BBI, na kwamba mwananchi hakuhusishwa kikamilifu.
‘‘Kwana uamuzi huo ni wa kihistoria majaji wameeleza bayana kuwa sheria haikufwatwa…mimi kama wakili nakubuliana nayo na ni kweli uhamasisho haukufanywa kikamilifu na mchakato mzima ulikuwa unaendeshwa na wanasiasa,’’ alisema.
‘‘Rais mwenyewe alikula kiapo kulinda katiba yeye mwenyewe hafai tena kuskuma mabadiliko yake,lazima tulinde katiba yetu na mapendekezo hayo mengi yalikuwa kinyume na sheria.’’ Aliongeza.
Kusonga ametaka wakenya kuwacha katiba kuhudumu na wanaisiasa wanafaa kuwa waaminifu na kuitumikia.
‘‘Kusonga mbele ni kwamba lazima tulinde katiba yetu ikiwa kuna wale wanaotaka kuibadilisha basi wafuate sheria.’’ Wambui alisema.