• Sat. Oct 12th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Marasta Kortini Kutafuta Haki ya Kutumia Bangi

May 17, 2021
814 300

Kundi la Marasta nchini Kenya limefika Mahakamani hii leo likitaka Marijuana yani Bhangi kuhalalishwa kwa matumizi ya kidini.

Wakitetea swala hili, katika ombi lao wamesema kuwa haki zao za uhuru wao wa kuabudu unakiukwa na wanaofaa kuruhusiwa kutumia marijuana na sio kujifanya haramu kwa kila mtu.

“Kifungu cha 23[1] na 165[3][b] na [d] cha katiba kina ipa Mahakama uwezo wa kuchunguza na kuamua iwapo haki na uhuru wa kimsingi wa wananchi umekandamizwa na kukiukwa au kutishiwa na sheria yeyote kuwa makossa na haiendani na katiba,” Ombi lao lilivyo soma.

Akizungumza nasi, Wakili anaye wakilisha kundi hili mahakamani amesema kuwa wanapigania haki za Marasta ili wapate uhuru wao wa kidini.

“Ombi la marasta ni kuwa waruhusiwe kupanda Marijuana nyumbani kwao na katika maeneo yao ya kuabudu. Sio kwa ajili ya burudani za jamii na umma,” Wambui alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *