• Fri. Mar 29th, 2024

Maelfu ya wakaazi wa Kisumu wajitokeza kumuona Rais Uhuru

Jun 1, 2021
349 300

Mamia ya Wakaazi wa Kaunti ya Kisumu wamekusanyika nje ya Uga wa Jomo Kenyatta ili Kusherehekea hafla za hamsini na nane za siku ya Madaraka.

Wananchi hawa waliweza kuanza kumiminika eneo Hilo kuanzia mida ya saa kumi na moja asubuhi kama walivyokuwa wameambiwa kufika mapema. Haya ndiyo maoni yao baada yao kuzungumza na Taarifa News;

“Kisumu ni kwetu na tumefurahi Sana kwa sherehe hizi kuletwa katika kaunti yetu Leo. Ila inasukitisha kwamba tumezuiliwa kuingia ndani licha yetu kufika mapema. Tuliambiwa tufike mapema ili turuhusiwe kuingia lakini sasa tunaambiwa hatutaingia kwa sababu hatuna kadi za mwaliko,”alisema Oscar Okoth Odera.

“Ni mara ya kwanza kumwona Rais Kenyatta na tumefurahi Sana. Lakini sasa haya mambo ya kutuambia eti lazima tuwe na kadi za mwaliko zinazltukasirisha Sana. Watuache tuingie ndani tumwone Rais wetu,”aliongeza Zachary Okumu.

“Kwa nini sasa sherehe hizi kuletwa huku na tuambiwe hatuwezi kuingia eti hatuna Kadi za mwaliko. Hata kama ni kununua Kadi tupo tayari kununua. Tuambiwe zinanunuliwa wapi. Ama zinapenwa wapi na nani. Hatutaki kuona hawa watu wanaoletwa na kuingizwa ndani na magari na sisi tupo hapa nje. Hatutoki hapa hadi turuhusiwe kuingia ndani,”alisema Oduor.

Aidha wananchi hao wameombwa kuwa watulivu na maafisa wa usalama. Wameambiwa watashughulikiwa na huenda wataruhusiwa kuingia.

Awali msemaji wa Ikulu, Bi Kanze Dena alikuwa amesema kuwa wale ambao watakuwa Kadi za mwaliko pekee ndio watakao ruhusiwa kuingia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *