• Sun. Jun 23rd, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Maafisa wa County Wahamishwa Baada ya Mzozo na Bosi Wao

Jul 8, 2021
239 300

Maafisa Wanne wa Kitengo cha ukaguzi katika Kaunti ya Nairobi (City Inspectorates) wamehamishiwa hadi kitengo Cha Utalii Biashara na Viwanda.

Hii ni baada kutokuwa na maelewano baina yao na Mkuu wa kitengo hicho Mark Leruk.

Inadaiwa kuwa mtafaruku baina yao ulikuwa kwa sababu zao za kibinafsi.

Wanne hao ni; Mkurugenzi Benjamin Omondi, Naibu wake Joseph Kipsang, Mkurugenzi Msaidizi Caroline Wairimu Njuguna na Mkurugenzi Msaidizi wa utekelezaji, Tom Seme.

“Tumekataa kuhusishwa katika ubadirifu unaoendelezwa na Leruk na baadhi ya Wawakililishi wodi. Haswa katika ubomozi unaoendelea. Hatutakubali, Leruk afisa aliyetumwa kwetu kutuharibia Ofisi,”alisema Mwakilishi mmoja wa Upinzani wodi wa Upinzani.

“Kulingana na kipengele Cha 72 katika Sheria za Kaunti Mwaka 2012, imeamuliwa mkahamishiwe kitengo Cha, Biashara, Utalii na Viwanda,” aliandika Musumba ambaye ni Kaimu Katibu wa Kaunti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *