• Sat. Apr 20th, 2024

Maafisa Sita Wa Polisi Kusalia Korokoroni Kwa Siku 14 Zaidi

Aug 17, 2021
306 300

Maafisa sita wa Polisi wanaohusishwa na mauaji ya Ndugu wawili,Benson Njiru na Emmanuel Mutura eneo la Kianjokoma kaunti ya Embu watazuliliwa kwa siku kumi na nne.

Maafisa hao, Benson Mbuthia, Consolata Kariuki, Martin Wanyama, Lilian Cherono na James Kariuki walifikishwa mapema hii Leo katika mahakama za Milimani mbele ya hakimu Daniel Ndugi.

Mahakama imeamua kuwa Maafisa hao wazuiliwe kwa siku kumi na nne Kama mawakili wa Mashtaka walivyoomba kwa Kuwa kesi hiyo ina msukumo wa Kitaifa.

“Siku kumi na nne sio nyingi…nakubaliana na Mawakili wa upande wa Mashtaka… Kesi hii inamsukumo wa Kitaifa . Wazazi wa vijana hao wanataka kujua aliyewauwa. Hili litawezekana tu iwapo maafisa wa Polisi watapewa muda kukamilisha uchunguzi,” Korti iliamuru.”

Ni muhimu kuwazuia kwa usalama wao wenyewe pia… Watu wana hasira kutokana na mauaji ya vijana hao na iwapo wataachiliwa, huenda kukazuka Vita,” aliongeza. Vijana hao waliozikwa siku ya Ijumaa waliuawa kwa njia ya kutatanisha wakiwa wamekamatwa na Polisi, siku kadhaa zilizopita baada yao kupatikana wakiwa wamekiuka sheria za kutokuwa nje nyakati za usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *