373 300
Wanakandarasi wanaosimamia ujenzi wa kivukio yaani flyover kilichopromoka hapo jana na kuwacha watu watano wakiwa wamejuruhiwa ndio wa kulaumiwa.
Hii ni kulingana na MCA wa Kangemi Paul Mahamba ambaye anasema wale kontrakta wameweka presha kubwa kwa wafanyikazi na hivyo kuwafanya kutomakanika vilivyo.
“Hao watu wanaowasimamia ujenzi ndio wa kulaumiwa wameweka wafanyikazi na presha ambazo hazina maana na hiyo imechangia kazi kufanyika chini ya viwango hitajika.” Mahamba alisema.
Wote watano walionusurika kifo walikimbizwa katika hospitali ya Kenyatta pahali ambapo wanaendelea kupokea matibabu.