• Sat. Sep 14th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

KNUT Motoni: Sossion Atimua Wanachama Afisini

May 24, 2021
520 300

Shughuli katika afisi za chama cha kutetea Masilahi ya Walimu (KNUT) zimelemazwa baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Sossion kuwazuilia Wanachama wa Kamati ya Uteuzi (NEC) nje ya Ofisi hizo.

Wanachama hao wa NEC walikua wamewasili afisini humo kwa mkutano wa kupinga uteuzi wa Sossion kama Katibu wa KNUT, na kutoa mwelekeo wa uchaguzi wa muungano huo.

Mvutano huo umelemaza shughuli za Wanachama hao ambazo zilikuwa zifanyike hii Leo katika ofisi hizo.

Katika taarifa zilizotufikia ni kuwa wakuu kadhaa katika chama hicho wametia fora ili kuhakikisha masharti hayo yakutowaruhusu kuingia yanatimilizwa.

“Wametufungia nje na kama sakafu zote zinasimamiwa na mishahara isiyopungua minne hii adhabu haitumikii walimu bali majivuno yake mwenyewe,” chanzo kilifunulia Taarifa News.

Sossion anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa kaimu mwenyekiti wa sasa Collins Oyuu ambaye yuko katika kambi moja na Stanely Mutai na naibu katibu mkuu wa kwanza wa Knut Hezborn Otieno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *