• Thu. Apr 25th, 2024

Kiongozi wa Wengi Bunge la Nairobi Guyo Kuwania Kiti Cha Ubunge Embakasi Central

Oct 26, 2021
300 300

Kiongozi wa waliowengi bunge la kaunti ya Nairobi ambaye pia ni mwakilishi wadi wa Matopeni Abdi Hassan Guyo Sasa ametangaza rasmi kuwa atawania kiti Cha ubunge Cha Embakasi Central …

Guyo amesema kuwa eneo bunge hilo liko nyuma kimaendeleo na Sasa Yuko na mipango kabambe kuhakikisha kuwa wananchi wa eneo hilo wanapata matunda ya kura zao.

Amesema atawania kiti hicho kupitia  chama cha Handshake lakini si UDA.

‘‘Nimechaguliwa mara tatu kule Matopeni hiyo inakuonesha nini?  nataka kutangaza leo kwamba nitawania kiti cha ubunge cha Embaksi Central 2022.’’ Guyo alisema.

‘‘Mtu asikuje hapa atuambie ati ametengeneza lami…barabara ni za  KURA na NMS na tumejua hizo taasisi za kujisimamia yeye mwenyewe atuambie amefanya nini na CDF  eneo bunge hili.’’ Guyo aliongeza.

Guyo tayari amepata ungwaji mkono kutoka kwa  MCAs wote wa Kayole Central wakiongozwa na Fred Okeyo wa Kayole South,John Kamau wa Komarock,Jeremiah Themendu wa Kayole Central ward na Samuel Ng’ang’a wa Kayole North.

‘‘Sisi tunajua tunaeleka wapi na tunajua maendeleo ya Guyo kwa sababu ni kiongozi wetu hata uko bunge..wacha tuweke wazi kuwa tunamuunga mkono kwa nia yake ya kuwania ubunge 2022.’’ Okeyo alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *