• Sat. Oct 12th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Kijana kutoka Familia za Kurandaranda Mitaani Afariki Njaa

Jul 23, 2021
576 300

Familia za kurandaranda mtaani (Chokoraa) wamwandamana hii leo wakiataka serikali kuwashughulikia baada mmoja wao kufariki ghafla kwa sababu ya kukosa chakula.

Wanasema kuwa mwendazake ambaye anatoka  mtaa wa  Mlango Kubwa  alifariki kutokana na njaa na hakupata usaidizi  wa haraka.

‘‘Alifariki  kwa sababu ya njaa huyu kijana shida tulikuwa nayo hatukupata chakula ya kumpa yeye… alikua anaomba wapita njia lakini hawakushughulikiwa,’’ Mmoja wao  aliambia  Taarifa News.

Alikimbizwa katika hospitali ya MSF lakini akakata roho baadae.

Stakabadhi zaonyesha kuwa aliletwa hospitalini MSF Mathare na Msamaria  mwema akiwa hai lakini akafa ghafla.

Familia za Kurandaranda Mtaani Wakichukua Mwili wa Mwenzao City Mortuary PICHA/JACKTONE LAWI

Mashirika ya kutetea haki za familia hizo yakiongozwa na Zero Street Families yametaka serikali kujitokeza na kusaidia familia hizo haswa maswala ya afya,lishe na hata makazi.

Fatma Mumbi ametaka wizara ya leba kujitokeza kuwasadia watoto hao ambao sasa wanafariki kutokana na njaa na kutopata matibabu.

‘‘Tumezika wengi huyu si wa kwanaza ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa wamepata huduma za afya,chakula na hata maakazi na pia tunashanga pesa ambazo hutengwa zao hutumika kufanya nini kwa sababu ni aibu kuzika kijana kama huyu kwa sababu ya njaa.’’

Mwili wake ulitolewa katika chumba hicho cha kuhifadhi maiti cha city na baadae akazikwa kule makaburi Langata.

Changamoto sasa ni kwa serikali kuhakikisha kuwa familia hizi zinapata usaidizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *