Kesi ya kuamuliwa kwa uhalalishaji wa matumizi ya Marijuana sasa itasikizwa tarehe ishirini na moja mwezi huu.
Jamii ya wana Rastafari ilipeleka kesi katika Mahakama ya Juu Nchini Mwezi uliopita wakitaka matumizi ya Marijuana kuhalalishwa kwa matumizi ya kidini.
Marasta hao walisema kuwa sheria inaenda kinyume cha katiba kwa kutohalalisha matumizi ya marijuana kwa sababu zao za kidini.
Wakili Shadrack Wambui ambaye anawawakilisha Marasta katika mahakama, amesema kuwa Jaji atakayesikiza kesi hiyo atakuwepo tarehe 21 mwezi huu na hamna haja ya wasiwasi.
”Tumepokea simu kadhaa Kulingana na swala hili wengi wakitaka kujua ni nini haswa inaendelea lakini nataka kuwaambia Marasta kuwa Jaji atakuwepo tarehe ishirini na moja mwezi huu na atapeana mwelekeo Zaidi,” alisema wakili Wambui.
Kesi hiyo ambayo ilipaswa kutajwa wiki iliopita ilihairishwa kwa kuwa Jaji Weldon Korir alikuwa katika shughuli zingine za kikazi.