• Thu. Jun 20th, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Kenya yapata Jaji Mkuu wa Kwanza Mwanamke

May 21, 2021
873 300

Martha Koome ameapishwa kuwa Mwanamke wa kwanza Jaji Mkuu katika historia ya Kenya.

Amechukua nafasi hii iliyowachwa wazi baada ya kustaafu kwa jaji Maraga.

Maraga atakumbukwa siku zote baada yake kubadili ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa mwaka 2017.


Sherehe hizi zimefanyika hii leo mwendo wa saa saba mchana.


“Rais Uhuru Kenyatta leo katika Ikulu ya Nairobi alishuhudia kuapishwa kwa Bi Justice Martha Koome Karambu kama mpya Jaji Mkuu wa Kenya na Rais wa Mahakama Kuu, na Jaji William Okello Ouko kama hakimu wa Mahakama Kuu,” Ikulu alisema kwenye Twitter.


Koome mwenye umri wa miaka 61 ameifanya taaluma yake ya mahakamani kwa muda wa miaka thelathini na tatu.

Uteuzi wake haukuwa na matata yeyote lakini wakili Fred Ngatia alikuwa ametoa madai kuwa mchakato wa kumteua Koome ulikuwa umechakachuliwa. Aidha Profesa Makau Mutua anayefanya kazi Marekani anatafuta maagizo ya kuishurutisha tume inayosimamia mahakama kutoa matokeo ya kila aliyehojiwa.


Majaji wengine wanohudumu katika mahakama ya upeo hawakutuma maombi ilikuteuliwa kama Jaji mkuu. Walionekana kuuchukuwa uamuzi huo kutokana na uhusiano Mbaya kati ya idara ya Mahakama na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *