• Fri. Mar 29th, 2024

Kampeni za Chama Cha Wahadhiri UASU wazidi Kupamba Moto

May 21, 2021
216 300


Huku uchaguzi wa chama cha wahadhiri nchini UASU ukiendelea kukaribia wagombea wameebdelea kuuza Sera zao katika matawi ya vyuo vikuu mbali mbali.

Kundi linaongozwa na katibu wa sasa Constantine Wasonga limekuwa Pwani kushawishi wahadhiri kuwapigia kura kwa awamu nyingine ya miaka mitano.

Onesmus Mutio wa kundi hilo anasema kuwa nia yao kuhakikisha kuwa maisha ya wahadhiri yamebadilika na ajenda yao ya kwanza kuhakisha utekelezwaji wa CBA zote zilipigwa sahihi.


“Tumekuwa Pwani tukitafuta kura chini ya kundi la Wasonga Fresh nia yetu ni kuhakikisha zile CBA zote zilizowekwa sahihi ikiwemo ile ya 2017-2021 imefanikishwa kikamilifu.” Alisema.


Wasonga anatetea kiti chake cha katibu mkuu huku Muga Kolale akitetea kiti chake cha uenyekiti.Onesmus Mutia anataka kiti cha mratibu mkuu wa chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *