502 300
Mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini amefikishwa katika kituo cha polisi katika kaunti ya Siaya baada yake kupatikana akishiriki ngono na Kondoo.
Inasemekana kuwa mwenye kondoo alikuwa amemfunga kondoo wake kwa malisho na kuondoka.
Aliporudi ndiposa alipata kondoo wake hayupo na alipomtafuta alimpata mwanaume aliyetambuliwa kwa jina John Omondi akiwa anashiriki ngono na kondoo wake.
Kwa usaidizi wa Umma uliojitokeza walimkamata mshukiwa na kumpeleka katika kituo cha polisi Siaya. Mshukiwa atafikishwa mahakamani na kushtakiwa baadaye.