• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Imwatok Arai Vijana Kukuza Talanta zao za Soka Makongeni

Jun 21, 2021
876 300

MCA wa wadi ya Makongeni Peter Anyule Imwatok sasa ametaka vijana kutumia talanta zao vyema katika nyanja za spoti kwani ndio njia ya kipekee kupigana na ukosefu wa kazi unayowakabili vijana sasa hivi mtaani.


Akiongeoa katika mashindano aliyoandana kwa ushirikiano na KARA kule Makongeni Imwatok ametaka vijana kuhakikisha kuwa wako mistari wa mbele katika ukuuzaji wa talanta zao na yeye kama mwakilishi ataendelea kushirikiana na mashirika mbali mbali kukuza talanta hizo katika wadi hiyo.


‘‘Nimefurahia kufika hapa Makongeni Grounds leo na washirika wetu kama Kara kutazama mashindano haya, na nataka kuhakikishia vijana wetu kwamba mimi sitawaacha tukipata mwanya na fedha tutaendelea kuandaa mashindano haya kwani leo nimefurahia jinsi mlivyojitokeza kushangalia timu zenu mbali mbali mtaani.’’ Imwatok alisema.


Katika mashindano ya jana klabu ya Maziwa County iliibuka na ushindi na wakatuzwa.


Mashindano ya jana ya Kandanda iligaragazwa katika uwanja wa Makongeni Grouds huku wakaazi zaidi ya 5000 wakihudhuria.


‘‘Iko poa tumecheza tumefurahia na hizo tona ndio inatuleta pamoja na tunataka kushukuru mheshimiwa Imwatok na mashirika kama vile Kara kukuja pamoja na kukuza talanta za vijana aendele na huo moyo ili vijana wawache kurandaranda mtaani.’’ Walisema walioshiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *