• Mon. May 20th, 2024

Hofu Yatanda Hospitali Ya Kunti Ya Homa Bay Wagonjwa Wakikosa Hewa

Jun 4, 2021
891 300

Wasiwasi umetanda katika Hospitali ya kaunti ya Homa Bay baada ya kuripotiwa ukosefu wa hewa kwa wagonjwa wakati ambapo visa vya Virusi vya Korona vina ongezeka.

Hospitali hiyo imekumbwa na uhaba wa hewa baada ya mitambo kufeli kusambaza hewa katika mitungi inayotumika hospitalini.

Haya yametumkia wakati Mbaya kwa kuwa idadi ya wanaokuja kutibiwa hostipitalini humo kutafuta matibabu ya viusi vya korona imeongezeka Zaidi.

Wale wanaowalinda wagonjwa wana wasiwasi Zaidi;

“Dada yangu anahitaji hewa sana lakini haipo,” alisema mwananchi mmoja.

Aidha, afisa wa afya katika kaunti ya Homabay Profesa Richard Muga amesema kuwa magari yametumwa katika kaunti za Nyamira na Kisumu kutafuta usaidizi.

“ Mashine zetu zilikumbwa na hitilafu kiasi , lakini tumetuma magari yetu katika kaunti za Kisumu na Nyamira kwa msaada wa hewa,” Alisema Muga.

Kando na Hewa, vitanda katika chumba cha wagonjwa maututi pia vimejaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *