• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Gari la Polisi Laua Kwenye Ajali Barabarani Ugunja Siaya

Aug 10, 2021
620 300

Mwanaume mwenye umri was miaka arubaini na tano Jumatatu aligongwa na gari la polisi eneo la Wang’Neno katika barabara za ya Ugunja-Ukwala kaunti ya Siaya.


Mwanaume huyo aliyetambuliwa kama Michael Odhiambo Oduor, alikuwa anatembea katika eneo hilo akielekea soko la Nzoia alipogongwa na gari lilokuwa linaelekea Ugunja kutoka Ukwala.


Kulingana na binamu yake,George Okech gari hilo lilikuwa likifuata gari aina ya Probox ajali hiyo ilipotokea.

Dereva wa gari hilo anadaiwa kusimama baada ya kumgonga Oduor lakini alipogundua kuwa alikuwa amefariki, alirudi kwenye gari na kuenda Ukwala.


Baada ya tukio hilo, Maafisa wa Polisi wa kituo cha Siranga ambao walifika katika eneo la ajali kabla ya kuwajuza wenzao was kituo Cha Ukwala na Ugunja ambao walikuja kuuchuka mwili huo na kupeleka kwenye makafani ya hospitali ya kaunti ndogo ya Ukwala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *