• Fri. Jun 21st, 2024

Taarifa News

Latest News Around the Globe

Duale Amuunga Rais Uhuru Mkono

Aug 12, 2021
281 300

Mbunge wa Garissa Mjini na aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la Kitaifa, Mheshiwa Aden Duale amempongeza Rais kwa kujaribu kuunganisha Upinzani kwa Mara ya Kwanza katika historia.

Katika mahojiano asuhi leo na runinga moja ya humu nchini, Duale amesema kwa Mara ya Kwanza Rais ameonyesha ukomavu wa Demokrasia na kuacha cheo chake ili kuunganisha Upinzani.

” Rais amewakutanisha pamoja viongozi wanaowakilisha maslahi ya Kikabila, namjua Rais nimefanya naye kazi kwa miaka nane iliyopita,”alisema Duale.

“Haijawahi kutokea katika historia yoyote ya Demokrasia iliyokomaa Rais kuwacha cheo chake na kuunganisha Upinzani,” aliongeza Duale.

Mbunge huyu amesema Ni wazi Kuwa mstakabali aliouchuwa Rais Kenyatta Ni wa aina yake. Hii ni baada ya Rais kuonyesha Nia ya kutaka mrithi wake awe wa kutoka Upinzani.

Mbunge wa Suba na mwakilishi wa Wachache katika bunge la kitaifa john Mbadi.

Duale alipeana mfano wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliyetaka mkewe Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma awe mrithi wake kwa Kuwa alikuwa amerejea nyumbani lakini Cyril Ramaphosa akampiku.

Duale alikuwa akizungumzia mkutano ambao Rais Kenyatta alikuwa nao katika ikulu ya Mombasa na Viongozi wa Upinzani. Duale alimkashifu Rais kwa kufanya mkutano na Viongozi hao akisema ni wawakilishi wa kabila tano zenye idadi kubwa nchini.

Aidha Mbunge wa Suba na Mwakilishi was wachahe katika bunge la Kitaifa, John Mbadi aliyekuwa katika mahojiano hayo alitofautiana na Duale kuhusiana na tofauti baina ya Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto.

Kulingana na Mbadi, uhusiano wa wawili hao, haukuzoroteshwa na salamu za mapatano baina ya Rais na Raila.

“Nafikiri Rais alimvumilia tu Naibu wake katika muhula was Kwanza. Uhusiano wao haukuzoroteshwa na makubaliano katika yake na Raila,”alisema Mbadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *