• Tue. Apr 23rd, 2024

Bunge la Nairobi lamulikwa na EACC baada ya ufichuzi

Aug 26, 2021
350 300

Vitengo vya Eacc,DCI na hata ya tume ya Kutathmini Mishahara ya Wafanyikazi wa Umma SRC Sasa vimepokea barua kutoka kwa mlalamishi fiche kutoka bunge la kaunti ya Nairobi Kuhusu njama ya wanasiasa wakuu na hata kaimu Karani bunge hilo kutaka kuwapandisha vyeo visivyo vibaraka na wanafamilia zao kinyume na sheria.


Katika nyaraka kadhaa kwenye barua hiyo,ofisi ya kaimu karani Adah Onyango amelaumiwa pakubwa kwa kupanga njama hiyo yeye pamoja na wanasiasa wengine wakuu bunge hilo.


“Hili ni kukuarifu kuwa kuna Njama ya kuwapandisha vyeo baadhi ya wafanyikazi bila kuzingatia mfumo unaotakikana kufuatia ombi la kaimu kirani kwa bodi ya bunge.” Barua ilisema.


Kulingana na barua hiyo kuna wafanyikazi ambao watanufaika kwa ajili ya zoezi hilo wakiwa ni Romeo Castro idara ya Huduma za kamati za bunge,Ahmed Makhoha ICT,Monica Muthami Sheria, Nancy Mutai,Brian Yambo idara ya Mawasiliano,Jared Osano,Erick Otieno bajeti,Kobia Marimba mkaguzi wa ndani, Christine Madara usalama,Osman Galgalo Usalama na Ramadhan Juma Kitengo Cha Usalama.


Mfichuzi huyo ametaka vitengo hivyo kuchukua hatua za haraka kuhakikisha zoezi hilo limesimamishwa mara moja kwani tayari kuna hofu kubwa bungeni miongoni mwa wafanyikazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *